By Khatimu Naheka

KOCHA wa Yanga, Nesreddine Nabi amemaliza tofauti zake na mshambuliaji wake Saido Ntibazonkiza akisema tayari kila kitu kipo sawa kisha akampa kazi moja tu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nabi alisema hana tatizo lolote na Saido kwasasa na kwamba kila kitu kimekuwa sawa baada ya mshambuliaji huyo kuwa nje ya kikosi hicho kwa muda.

Nabi alisema amefanya kikao kirefu na mshambuliaji huyo mkongwe na kila kitu sasa kipo sawa lakini pia amempa nafasi ya raia huyo wa Burundi kujieleza mbele ya wachezaji wenzake akiwa kama mchezaji mzoefu.

SOMA: Ishu ya Saido ipo hivi…

“Sina matatizo yoyote sasa na Saido, yeye ni sehemu ya hii timu na tuko naye ingawa hakusafiri. Kila kitu kimemalizika, tunatakiwa kuwa na nidhamu sawa kwa kila mmoja katika timu hii,” alisema Nabi na kuongeza;

“Nimezungumza na Saido na tumekubaliana lakini pia aliongea na wenzake wote wameelewana, sasa yuko na sisi katika safari moja ingawa tulimuacha katika safari hii ya Songea.

Advertisement

“Kazi aliyonayo Saido ni kupigania nafasi yake kwenye timu, nikiona anaimarika kama ninavyotaka nitampa nafasi, sina tatizo na mchezaji ambaye naona anaweza kusaidia hii timu, tunahitaji mafanikio na kazi hiyo itafanywa na sisi makocha na wachezaji,” alisema.

Saido hajaonekana katika mechi zote tatu za kwanza msimu huu huku ikitajwa kwamba mshambuliaji huyo alikuwa na tofauti na kocha Nabi.News Source link

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles