More
  - Advertisement -

  Naibu Waziri aomba ushirikiano baina ya Viongozi Wakuu wa Wizara,Watendaji na Watumishi

  -

  - Ad Keep reading below -

  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Philipo Gekul ameomba ushirikiano baina Viongozi Wakuu wa Wizara, Watendaji na Watumishi wote wa Wizara ili kutekeleza majukumu ya Wizara hiyo kimamilifu kulingana na Miongozo ya Serikali, Maelekezo ya Mheshimiwa Rais na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hatimaye matarajio ya wananchi yaweze kufikiwa.

  Mhe. Gekul ameyasema haya alipowasili rasmi leo kwenye Ofisi yake mpya eneo la Mji wa Serikali- Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kwenye nafasi hiyo hivi karibuni akitokea Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambako alikuwa akihudumu kwa nafasi hiyohiyo.

  - Ad Keep reading below -

  “Mheshimiwa Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara, madaraka haya tuliyopewa ni sawa na makoti ya kuazima hivyo tuna kila sababu ya kumtanguliza Mungu na kuimarisha ushirikiano ili kuleta matokeo tarajiwa kwa wananchi wetu wakati tunatekeleza majukumu yetu ya kila siku” amesisitiza Mhe. Gekul Amemshukuru Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumwamini na kumrejesha tena kwenye nafasi hiyo pamoja na viongozi wote Wakuu wa Wizara hiyo ambapo ameongeza kuwa hali hiyo itarahisisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa ufanisi kwa kuwa watendaji wote wamerejeshwa na wanauzoefu wa kutosha.

  ALSO READ  Give Nigerians AK-47, they won’t run from bandits – Fani-Kayode tells Defence Minister
  ALSO READ  Dlamini-Zuma issues new lockdown laws – with jail threats for alcohol offences

  Amemhakikishia Waziri Bashungwa kufanya kazi kwa bidii ya kumshauri na kumsaidia kwa kadiri ya uwezo wake wote kama msaidizi wake.

  - Ad Keep reading below -

  Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Watumishi wote kuwa na mshikamano wa hali ya juu ambapo amesisitiza watumishi wasisubiri kusukumwa na Katibu Mkuu na badala yake wachape kazi ili kukidhi dhamira ya Mhe. Rais ya kuwatumikiwa wananchi kikamilifu.

  “Napenda kusema tukigundua mahali popote kwenye Wizara yetu hakuna ushirikiano tutachukua hatua mara moja maana hiyo itakuwa ni hujuma kwa taifa”amefafanua Mhe. Bashungwa

  Amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kumwamini na kumteua tena kuendelea kusimamia Sekta zilizo chini ya Wizara hiyo pia kumteua Mhe. Gekul kuja kuongeza nguvu katika kutekeleza na kumuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kutekeleza Ilani ya CCM na hotuba aliyoitoa awali kama mwongozo kwa Watendaji wote wa Serikali.

  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi amemshukuru Mhe.Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kwa mara nyingine kuwa Katibu Mkuu na kumwahidi kushirikiana na Viongozi na Watumishi wote kutekeleza majukumu ya Wizara kwa weledi na kuzingatia taaluma.

  ALSO READ  Watu 9 wakiwemo Askari wa Jeshi la Polisi washikiliwa kwa tuhuma za Rushwa
  - Ad Keep reading below -

  Akizungumza kwenye Kikao cha Menejimenti ya Wizara hiyo mara baada ya kupokea maelekezo ya Waziri Bashungwa, Dkt. Abbasi amesisitiza watendaji wa Wizara kutoka na kuwa jirani na wadau wa sekta zilizochini ya Wizara hiyo kwa kuwa wanahitaji kulelewa kwa karibu. 

  ALSO READ  Kiongozi wa ISIS nchini Iraq auawa katika shambulizi la anga

  Amesema jukumu la Wizara ni kuzisimamia sekta zilizo chini ya wizara hiyo kikamilifu kwa weledi ili kupata matokeo chanya kwa kuwa nchi yetu imebahatika kuwa na wasanioi wenye vipaji na vipawa vingi kinachotakiwa ni usimamizi madhubuti.

   

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Chicago to Release Video of Cop Fatally Shooting 13-Year-Old | Illinois News

  By DON BABWIN, Associated PressCHICAGO (AP) — Body camera footage of a Chicago police officer fatally shooting a 13-year-old boy last month will be...

  Mother sues Nsambya hospital over negligence, seeks Shs 400m

  Rose Namara accuses Nsambya hospital of medical negligence ...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -