Swahili News

Nini Maana ya Katiba ya Nchi na umuhimu wake?

Katika nchi yoyote msingi wa uendeshaji wa nchi unategemea Katiba. Katiba ni sheria kuu au sheria mama katika nchi yoyote. Sheria nyingine zote zinategemea au zinatungwa kwa mujibu wa katiba, wakati mwingine katiba hutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kijamii kati ya watawala na wananchi (watawaliwa).

Ni makubalianao ya wananchi husika juu ya ni jinsi gani taratibu za kanuni za uendeshaji wa mambo mbali mbali katika nchi yao unapaswa kuwa.

Ni muafaka wa Kitaifa juu ya misingi mikuu ya kuendesha nchi. (Maneno ya Pro.Shivji katika kongamano tarehe 15/1/2011Dar es Salaam.)

Historia Ya Katiba Katika Nchi Zilizotawaliwa na Wakoloni

Kwa ujumla nchi nyingi hasa zile zinazoendelea zina katiba zilizoandikwa.nyingi kati ya katiba hizo zilitungwa na kurekebishwa na watawala wa kikoloni, na nyingine zilitungwa baada ya makubaliano na tawala za kikoloni kabla ya kuondoka.Katiba hizo ni maridhiano ambayo yalilinda maslahi ya pande zote mbili:
(1)Tawala za kikoloni zilizokuwa zikiandika.
(2)Nchi iliyokuwa ikipata uhuru

“Katiba nyingi katika nchi zilizoendelea zina uhusiano na Katiba na Tawala za kikoloni.

Historia ya katiba hapa Tanzania pia ina uhusiano na tawala za kikoloni zilizokuwa zinatawala kabla ya uhuru
Historia Ya Mabadiliko Ya Katiba Tanzania 1961 Katiba ya kwanza ya uhuru iliyowekwa na Waingereza (Independence Constitution).

1962Katiba ya Jamhuri (The Republic Constitution) iliitambua Tanganyika kama Jamhuri na ilipunguza madaraka ya Bunge(Imewekwa na Waingereza). 1965 Iliwekwa katiba ya muda (The Interim Constitution) 1977 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitungwa na Bunge Maalum (Constitutional Assembly), (wananchi hawakuhusishwa). Angalia HAKI toleo la 5 uk.10).

Prof. Issa Shivji anabainisha haya pia katika Kongamano la Katiba lililoandaliwa na wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumamosi tarehe 15/1/2011 angalia Gazeti la

1961 Katiba iliruhusu mfumo wa vyama vingi, na Vyama vifuatavyo vilisajiliwa:TANU, United Tanganyika Party(UTP), African National Congress(ANC), The Peoples Democratic Party(PDP), Peoples Convertion Party(PNP), National Enterprise Party(NEP), All Muslim Nationalist Union of Tanganyika(AMNUT), African Independence Movement(AIM).

  1. 1963 Halmashauri Kuu ya TANU ilipitisha maamuzi kufanya Tanganyika kuwa nchi ya chama kimoja.
  2. 1965 Sheria ya chama kimoja iliingizwa kwenye Katiba.1977Haki za binaadamu ziliingizwa rasmi katika Dibaji.
  3. 1984 Katika katiba ya Jamhuri haki za binadamu ziliingizwa rasmi katika katiba.
  4. 1992 Katiba iliruhusu tena mfumo wa vyama vingi kwa shinikizo la nchi za kibeberu

Katika kitabu: Elimu ya Demokrasia shirikishi (Kitabu kilichotolewa na CTP Dom uk.7) chasema hivi:
“Wanasayansi wa mambo ya siasa wanaelekea kukubali kwamba demokrasia ya vyama vingi imeingizwa toka nje kwa kutokana na masharti ya kupata misaada ya fedha”.

Mambo Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba(1977) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
1. Mfumo Wa Demokrasia

Nini maana ya Demokrasia? Ni neno lenye asili ya kigiriki (Demo-Crates) yaani utawala wa watu.
“Ni mfumo wa kuendesha serikali ya watu iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu, madaraka na mamlaka, ya mwisho ya serikali hiyo yako mikononi mwa watu”

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, sehemu ya pili, Serikali na watu, sheria ya 1984 na.15, 16.6, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na Haki za Kijamii na kwa hiyo:
a) Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii.
b) Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi serikali itawajibika kwa wananchi
Mamlaka Ya Kutunga Sheria Yako Mikononi Mwa Watu

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kifungu 64 (1): Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo yote yahusuyo Tanzania Bara yatakuwa mikononi mwa Bunge
Kifungu 106 (3): Madaraka yote ya kutunga sheria katika zanzibar katika mambo yote yasiyo mambo ya muungano yatakuwa mikononi mwa baraza la wawakilishi wa Zanzibar.

3. Mfumo Wa Kutenganisha Dini Na Mamlaka Ya Nchi (Siasa)
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kifungu 19 (2): Bila kuathiri sheria zinazohusika za jamhuri ya muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuia za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi

Katika katiba toleo la 2005 ibara ya 3:
3 (1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya Kidemokrasia na ya Kijamaa, isiyokuwa na Dini yenye kufuata Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa

Mfumo Wa Kufuata Siasa Ya Ujamaa Kwa Mujibu Wa Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano
Kifungu cha 9: Lengo la katiba hii ni kuendesha ujenzi wa jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu wa amani kutokana na kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika jamhuri ya muungano.

Mfumo Wa Kukataza Kuanzishwa Chama Cha Siasa Chenye Lengo La Kukuza Dini

Kwa mujibu wa katiba kifungu 20 (2): Kwa kujali masharti ya ibara ndogo (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba au sera yake:
A) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya: I) imani au kundi lolote la dini. Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 26 (1): Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii katiba hii na sheria za jamhuri ya muungano. Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri kifungu 45 (1): Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:

A) kutoa msamaha kwa mtu yoyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote na aweza kutoa msamaha bila masharti au kwa masharti kwa mujibu wa sheria.
B) kumwachilia kabisa au kwa muda maalumu mtu yeyote aliyehukumiwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum.
C) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu.
D) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yote.

Uhuru Wa Kubadilisha Dini Anayotaka
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 19 (1): Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake. Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 67 (3): Mtu hataweza kugombea uchaguzi kuwa mbunge wa kuwakilisha jimbo la uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu wowote ikiwa wakati huo yeye amesimama katika uchaguzi kugombea kiti cha Rais, wala hataweza kugombea uchaguzi kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo wowote ikiwa yeye ni Rais.

Mfumo Wa Vyama Vingi Vya Siasa
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 3 (1): Jamhuri ya muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kiongozi Mkuu Wa Nchi (Rais) Kuwa Juu Ya Sheria
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 46:
(1): wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashtaka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
(2) wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosea kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais

Matumizi Ya Mapambano (Jihadi) Yanakataliwa: Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 20 (21): Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba na sera zake: (c) kinakubali na kufungamana na matumizi ya nguvu au mapambano kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Haki ya Usawa, kifungu 12(4): Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.

Kifungu 12 (5): Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno kubagua maana yake ni kutimiza haja, haki, au mahitaji mengineyo kwa watu mbali mbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahali walipotokea, maoni ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali ya maisha kwa namna ambapo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa dhaifu au duni au kuwekewa vikwazo au masharti ya upingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa auwanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima isipokuwa kwamba neno kubagua halitafafanuliwa kwa maana ambayo itazuia serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 18 (2): Bila kuathiri sheria zinazohusika za jamhuri ya muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada au kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi na shughuli za uendeshaji wa jumuia za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 9: Mamlaka ya nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha: (e)kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi, anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli ya halali inayompatia mtu riziki yake.

Neno Usawa
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 13(1): WATU WOTE MBELE YA SHERIA NA WANAYO HAKI, BILA YA UBAGUZI WOWOTE, KULINDWA NA KUPATA HAKI SAWA MBELE YA SHERIA.

Vile vile kifungu 12(1): BINAADAMU WOTE HUZALIWA HURU NA WOTE NI SAWA.
Neno Haki Ya Kuishi. Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu (1): Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kwa uhuru. Hii imetafsiriwa kwamba hata aliyeua asiuliwe kwa sababu ana haki ya kuishi.
Neno Haki Ya Kumiliki

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 24 (1): Bila kuathiri masharti ya sheria za nchi zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria. Imefasiriwa kipengele hiki kwamba mtu ana haki ya kugawa urithi, atakavyo yeye maadam ni mali yake.

Kufutwa Adhabu Ya Viboko
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 136(e): Ni marufuku kwa mtu kuteswa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha. Mahakama kuu Dodoma katika kesi ya Thomas s/o Mjengi Vrs.R, Dodoma High Court Criminal appeal Na.28/1991 hapo tarehe 23/6/1992 ilihukumiwa kuwa adhabu ya viboko na adhabu ya kima cha chini cha kifungo cha miaka 30 kwa kosa la unyanganyi ni kinyume cha Ibara ya 13(6) (e) ya Katiba yetu.

Tunapojiandaa kwenda kusaka/kutafuta maoni kutoka kwa wananchi ili kutunga/kuunda Katiba Mpya,ni muhimu kila Mtanzania awe na ufahamu kuwa Katiba nini na Faida zake,nimeweka huu uzi ili watu wajifunze.

Elisante Yona – Kutoka Same Kilimanjaro.

Source
Source

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.