Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Njombe: Mama atuhumiwa kumuua mtoto wake wa miaka 3 kwa kumkata na shoka

Advertisement Scroll To Keep Reading

Advertisement Scroll To Keep Reading

Na Amiri Kilagalila,Njombe.

Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia mwanamke aliyefahamika kwa jina la Vaileth Chaula (30) mkazi wa kijiji cha Mkongomi kata ya Kidugala wilayani Wanging’ombe kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaa Azgad (3) kwa kumkata na shoka kichwani na kupelekea kifo chake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issah amesema kwa mujibu wa maelezo ya wanandugu mwanamke huyo alikuwa na matatizo ya akili.

Alisema miezi michache iliyopita mwanamke huyo akiwa Makambako alipokuwa ameolewa  alipatwa na matatizo ya akili na kurudishwa nyumbani kwao kwa wazazi wake ili apatiwe matibabu.

Alisema akiwa na mtoto huyo ambaye alionekana kudeka mama yake huyo aliona kuwa anasumbuliwa na mtoto huyo hivyo alichukua shoka ili kumkata kata mtoto huyo.

“Huo ni ukatili tunaita ingawa huyu mama ni mgonjwa lakini sasa sheria haisemi namna hiyo” alisema Issah.

Alisema mwanamke huyo anashikiliwa na jeshi hilo likiwa linasubiri kukamilika kwa baadhi ya mambo ili aweze kufikishwa mahakamani.

 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.