Utawala wa Rais Joe Biden umeweka wazi nyaraka za Idara ya upelelezi ya Marekani FBI zilizoihusisha serikali ya Saudi Arabia na watuhumiwa waliohusika na mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11.

Nyaraka hizo ambazo zilikuwa siri hadi sasa, zinaonyesha uhusiano kati ya Omar Bayoumi, wakati huo akiwa mwanafunzi lakini anashukiwa kuwa jasusi wa Saudi Arabia, na wapiganaji wawili wa Al-Qaeda walioshiriki katika njama ya kuziteka nyara ndege za abiria na kuzigongesha katika majengo mjini New York na Washington. 

Kulingana na mahojiano ya mwaka 2009 na 2015 na chanzo ambacho kimewekwa kuwa siri, nyaraka hiyo inaelezea mawasiliano kati ya Bayoumi na watekaji nyara wawili Nawaf al-Hazmi and Khalid al-Midhar, baada ya wawili hao kuwasili mjini Carlifonia mwaka 2000 kabla ya mashambulizi hayo. 

Chanzo hicho kiliiambia FBI kuwa Bayoumi, kando na kutambulishwa kuwa mwanafunzi, alikuwa ni mtu mwenye hadhi ya juu katika ubalozi wa Saudi.Nyaraka hiyo imetolewa baada ya Rais Joe Biden kushinikizwa na familia za jamaa waliouwawa katika shambulio hilo, ambao wameishtaki Saudi Arabia kwa kuwa mshirika kwenye njama hiyo.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles