Hatua hiyo ya kuuchagua mji wa Rais Uhuru Kenyatta kwa kuanza kampeni, ni ishara, huku rais akiwa anataka kuwavuta wafuasi wake waunge mkono muungano wa Azimio la Umoja wa Odinga kufuatia makubaliano yao waliyofikia Machi 2018.

Rais Kenyatta ameonyesha kuunga mkono ugombea wa waziri mkuu wa zamani katika mikutano ya hadhara kadhaa na baadhi ya washirika wa rais wametajwa hivi karibuni katika timu ya kampeni ya Odinga.

Siku ya Alhamisi, alikuwa mwenyeji wa wanachama Rafiki wa Bunge la Taifa na Baraza la Seneti katika chakula cha mchana, kuwashukuru kwa kupitisha marekebisho ya sheria za vyama vya siasa, inayotaka kuondoa vikwazo vya sheria dhidi ya ushiriki wa muungano wa Azimio katika uchaguzi wa mwaka huu.

Pia alitumia hafla hiyo kuwashawishi Maseneta kupitisha (marekebisho) ya mswaada wa vyama vya siasa kabla ya kupitishwa kuwa sheria.

Kupitishwa kwa Mswaada huo katika Bunge la Taifa kulicheleweshwa na mjadala wa wabunge wenye mafungamano na chama kilichojitenga cha Makamu wa Rais William Ruto cha United Democratic Alliance (UDA), wanaoona huo ni sehemu ya mpango wa Rais Kenyatta kusimamia kupatikana mrithi wake.

End

Tagged in: