Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Papa Francis aitolea mwito Hungary "kumkumbatia kila mtu"

Advertisement Scroll To Keep Reading

 

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis leo Jumapili ameihimiza Hungary “kumkumbatia kila mtu,” kauli yake ikionekana kumlenga Waziri Mkuu Viktor Orban. 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Papa Francis alikutana na Orban, ambaye sera zake za uhamiaji zinakinzana na wito wa kiongozi huyo wa kidini anayeunga mkono ujumuishaji na kuwakaribisha wahamiaji wanaotafuta maisha bora Ulaya.

 Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani mwenye umri wa miaka 84 anayefanya ziara ya siku nne Ulaya ya kati, alikaa mjini Budapest kwa masaa saba pekee kabla ya kuelekea nchi jirani ya Slovakia. 

Vatican na maafisa wa Hungary wamesisitiza kuwa Papa Francis hajaidharau Hungary kwa kukaa muda mchache nchini humo, na kwamba serikali ya Hungary ilimualika kwa ajili ya ibada maalum ya kutoa shukrani. Orban amejitokeza wazi kuwa mtetezi wa tamaduni za Kikristo barani Ulaya ambazo haziingiliana na tamaduni za wahamiaji ambao wengi wao wanatokea katika mataifa ya kiislamu.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.