More
  - Advertisement -

  Pochettino afunguka suala la Mbappe kukosekana leo

  -

  - Ad Keep reading below -

  Kocha wa PSG, Mauriccio Pochettino amesema suala la nyota wake tegemezi, Kylian Mbappe kucheza ama kutocheza mchezo wa saa 4:00 usiku wa leo Mei 4, 2021 dhidi ya Manchester City kwenye nusu fainali ya mkondo wa pili bado halijafanyiwa maamuzi.

  Akizungumza kuhusu hali ya Mbappe, Pochettino amesema, “ Tunahitaji kumfanyia vipimo Mbappe. Ataendelea na mazoezi binafsi na tutaangalia kama anaweza kuwa sehemu ya timu. Kuna muda umesalia na tutaamua kama atakuwepo”.

  - Ad Keep reading below -

  Mbappe amejipambanua kama mchezaji tegemezi kwenye safu ya ushambuliaji ya PSG, kwani amefanikiwa kufunga mabao 8 na kutengeneza 3 kwenye michezo 10 aliyocheza kwenye michuano ya klabu bhingwa Ulaya, utofauti wa mabao 2 na kinara wa ufungaji Braut Haaland.

  Kwa upande wa michuano yote, Mbappe ameshaifungia PSG mabao 37 na kutengeneza mengine 10 sawa na kuhusika kwenye mabao 47 katika michezo 43 aliyoichezea klabu yake hiyo ya matajiri wa jiji la Paris nchini Ufaransa kwenye michuano yote.

  - Ad Keep reading below -

  Kuzungumzia namna mchezo utakavyo kuwa na maandalizi yake, Pochettino amesema, “Tunahitaji kuwa tayari kuteseka kwenye nyakati fukani kimchezo, na tukipata nafasi tunapaswa kuwa watumiaji wazuri wa nafasi na kuchangamka”

  ALSO READ  Waziri Mkuu wa Uingereza aahidi kutoa chanjo za ziada kwa nchi maskini katika mkutano wa G7
  ALSO READ  Taasisi za Nunuzi wasisitizwa kuandaa mpango wa ununuzi ili mahitaji yapatikane kwa wakati

  “Ni mchezo ambao, dakika 90 zilimalizika tunapswa kupata ushindi wa zaidi ya mabao mawili. Kama tunahitaji kwenda fainali babsi, tunapaswa kupata ushindi wa utofauti wa mabao mawili . Hilo ndilo lengo na tutaenda kujaribu”.

  Pochettino amesisitiza kuwa hawana budi kujitoa muhanga ili kupindua matokeo, “Wanafaiada ya mabao 2-1, na hatuna budi kujitoa muhanga. Tunapaswa kuwa majasiri, tutumie akili, tuamini na tuoneshe ubora wetu uwanjani”. Alimalizia hivyo, Pochettino.

  PSG wanatazamiwa kumkosa kiugo wake mkabaji, Idriss Gueye Gana ambaye anakosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja kufuatia kadi nyekundu aliyooneshwa kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

  - Ad Keep reading below -

  Manchester City hawana wachezaji wenye majeraha isipokuwa mlinzi chipukizi, Erick Garcia ana sumbuliwa na ugonjwa wa Malaria akiwa ndiyo mchezaji pekee atakayekosekana.

  PSG ataingia na kumbukumbu yakupoteza mchezo wake wa mwisho kwenye dimba la Etihad, kwa kufungwa bao 1-0 na kuondoshwa kwenye hatua ya robo fainali Aprili 2016 kwa bao pekee la Kevin De Bruyne.

  ALSO READ  RC Makonda amuonya mkandarasi wa mradi wa ujenzi na maboresho ya mto Ng’ombe
  ALSO READ  RC Makonda amuonya mkandarasi wa mradi wa ujenzi na maboresho ya mto Ng’ombe

   

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Postpone LG election to avoid another legal gymnastics – ex-Oyo Gov, Alao-Akala tells Makinde

  A former Governor of Oyo State, Chief Christopher Adebayo Alao-Akala, has advised the incumbent Governor, Engineer Seyi Makinde, to without wasting more time, postpone...

  Group of restaurants planning to open on June 2nd in breach of Covid restrictions

  A group of restaurants and cafés is planning to reopen on June 2nd in breach of Covid-19 regulations. The social media campaign has identified June...

  Leicester 2-4 Newcastle: Player ratings

  Leicester City's hopes of holding on to a place in the top four were dealt a huge blow as they were thumped 4-2 by...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -
  %d bloggers like this: