AfricaSwahili News

Polisi wenye mabomu na mbwa wazuia kongamano

Kongamano la Chama cha Siasa cha CHADEMA la kudai Katiba mpya lililokuwa lifanyike leo Jijini Mwanza, limeshindwa kufanyika baada ya polisi waliobeba mabomu ya machozi, silaha za moto pamoja na magari yenye mbwa kutanda katika eneo la hoteli mahali ambapo kongamano hilo lingefanyika.

Hapo jana Julai 20, 2021, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, alipiga marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima katika mkoa huo kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa hatari wa Corona.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi, ziligonga mwamba baada ya kupigiwa simu mara kadhaa na kutopokea, lakini hivi karibuni RPC huyo alisema hatoruhusu kufanyika kwa mikutano isiyokuwa na vibali.

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.