By Juma Mtanda

Morogoro. Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi amewataka Mawakili wa serikali Ofisi ya Taifa ya Mashtaka pamoja na waendesha mashtaka wateule na wapelelezi na maofisa wa wanyamapori na misitu kuwa na weledi katika kazi hizo kwani wahalifu wa eneo hilo wana mtandao mkubwa na fedha nyingi.

Akizungumza leo Oktoba 18 na maafisa hao katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tano, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagama Kabudi amesema umakini mkubwa unahitajika kwa wahalifu hao.

“Makosa ya ujangili na wizi wa mazao ya misitu yanayofanywa na watu wenye fedha na wenye mtandao mkubwa. Katika utamaduni wetu kwetu meno ya tembo hayana thamani kubwa, lakini nje yana thamani hivyo ni lazima kuwa makini katika kukusanya ushahidi,” amesema Profesa Kabudi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), Sylvester Mwakitalu amesema kuwa kumekuwa na ongezekola makosa ya wanyapori na mazao ya misitu nchini hivyo mafunzo hayo kwao yana tija katika kuwanoa kundi hilo ili kuwa na uweledi zaidi.

Akifafanua ukubwa wa tatizo hilo, Mwakitalu amesema katika kikao cha Mahakamu ya Rufaa kilichoanza Musoma mkoani Mara, imebainika kuwa kuna kesi 18, ambapo kesi 14 kati yake ni za wanyamapori na misitu.

Naye Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Makosa ya Mazingira na Maliasili wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Rosemary Shio alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo kwa kuwapatia ujuzi utakao wawezesha kupeleleza na kuendesha kesi za wanyamapoti na misitu kwa weledi na uadilifu.

Advertisement

Katika mafunzo hayo kwa washirika hao watanolewa na majaji watatu kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania akiwemo na Jaji George Masaju, Jaji Gerson Mdemu, Jaji Amour Khamis.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles