AfricaSwahili News

Rais Biden asisitiza uhusiano imara kati ya Marekani na Ulaya

 

Rais Joe Biden wa Marekani ameondoka nchini humo kuelekea Uingereza ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kigeni huku akisisitizia mahusiano imara kati ya Marekani na Ulaya, kabla ya mkutano wa kilele kati yake na kundi la mataifa saba yenye nguvu kiuchumi la G7, washirika wa jumuiya ya kujihami ya NATO na mkutano wa ana kwa ana na rais wa Urusi, Vladimir Putin. 

Biden amewaambia waandishi wa habari alipokuwa akiondoka Washington kwamba ziara yake itamuonyesha Putin na China kwamba kuna mahusiano imara kati ya Marekani na Ulaya. 

Ziara ya Biden inaanzia Uingereza kwa ajili ya mkutano huo wa G7 unaoanza siku ya Ijumaa, na baadae Brussels kwa ajili ya mkutano na NATO na Umoja wa Ulaya na kumalizia Geneva atakapokutana na Putin, Jumatano ijayo, ingawa kuna matumaini finyu. 

Katika hatua nyingine, Biden amesema anatarajia kutangaza mpango wa dunia wa chanjo dhidi ya virusi vya corona baadae hii leo.

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button