Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kwamba ufichuzi wa nakala za ‘Pandora papers’ utaimarisha uwazi wa umiliki wa fedha unaohitajika nchini Kenya na duniani kwa jumla.

Ufichuzi mkubwa wa nakala za kifedha uliofanywa na muungano wa waandishi wapelelezi ICIJ, unaonesha kwamba rais Kenyatta na familia yake, kisiri walimiliki mtandao wa kampuni zilizofunguliwa katika nchi za kigeni kwa miongo kadhaa.

Kulingana na mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi , Bwana Kenyatta amesema kwamba usafirishaji wa fedha , mapato yaliopatikana kwa njia za uhalifu na ufisadi ulifanyika katika mazingira ya siri na giza.

Rais Kenyatta aliongezea kwamba kitakachofuatia baada ya ufichuzi wa nakala hizo za Pandora na ukaguzi , utaondoa usiri na giza kwa wale ambao hawawezi kuelezea mali na utajiri wao.

Kulingana na ufichuzi huo , uwekezaji uliofanywa katika nchi za kigeni na familia hiyo unashirikisha kampuni moja yenye hisa na dhamanazenye thamani ya $30m, wakfu ambao mamake , Ngina Kenyatta wameorodheshwa kuwa wamiliki na kampuni moja ya kigeni ambayo haikuweza kugunduliwa wamiliki wake licha ya kwamba ilihusika kununua nyumba moja katikati ya mji wa London ambayo kwa sasa ina thamani ya dola milioni 1.3 million.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye yuko nje ya nchi ameahidi kutoa taarifa kamili atakaporudi.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles