By Florah Temba

Moshi. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro, ambapo atazindua miradi, kuweka mawe ya msingi na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari,  leo jumatano Oktoba 13, 2021, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, amesema Rais Samia, atawasili mkoani humo Oktoba 14 jioni na kuanza ziara oktoba 15.

Amesema akiwa mkoani humo, atazindua barabara ya lami ya Sanya Juu – Elerai yenye urefu wa kilomita 32 iliyogharimu zaidi ya Sh60 bilioni na kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi ambayo inatarajiwa kugharimu Sh12 bilioni hadi kukamilika.

Kagaigai amesema, Rais pia akiwa Kilimanjaro ataweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Rau ambalo lilisombwa na maji ya mvua mwaka juzi, linalojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh900 milioni.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi ambapo Rais Samia atahutubia.

Amesema Oktoba 16, Rais atashiriki jubilei ya miaka 50, ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).

Advertisement

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles