Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Rais wa Marekani azungumza na rais wa China baada ya miezi saba

Advertisement Scroll To Keep Reading

Rais wa China Xi Jinping amezungumza na rais wa Marekani Joe Biden kwa mara ya kwanza ndani ya miezi saba.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Taarifa ya Ikulu ya Marekani ilisema viongozi hao wawili ilizungumzia majukumu ya mataifa hayo mawili katika kuhakikisha mashindano hayasababishi migogoro.

Hii ni mara ya pili kwa marais hao kuzungumza kwenye simu tangu rais Biden aingie madarakani.

Uhusiano wa Marekani na China umekuwa si mzuri kutokana na mvutano wa kibiashara na janga la corona.

“Viongozi hawa wawili walikuwa na mazungumzo ya kina katika maeneo ambayo wana maslahi nayo,”taarifa ya Ikulu ya Marekani ilieleza.

Shirika la utangazaji la China CCTV lilisema mazungumzo hayo ya simu yalilenga kukubaliana kuwa na mikakati ya mawasialiano na suala la kuafikiana.

“Si China na Marekani wanaweza kukabiliana na mahusiano yao bali ni kwa ajili ya siku za usoni kwa dunia nzima ,” alisema Xi, kwa mujibu wa taarifa ya CCTV .

Mtangulizi wa bwana Biden, Donald Trump alikuwa anazungumza na bwana Xi wakati alipoingia madarakani.

 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.