Mchezaji wa Biashara United, Ramadhan Chombo (Redondo) amefanikiwa kupata zawadi ya mchezaji bora katika michezo minne iliyocheza timu hiyo mwezi Septemba. Chombo amepokea mfano wa cheki yenye thamani ya sh 300,000/- kutoka kwa wadhamini wao Jet & Sons baada ya kuchaguliwa na benchi la ufundi pamoja na mashabiki wa timu hiy. Biashara imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Jet & Sons, ambapo pamoja na mambo mengine utawezesha kutoa kiasi cha sh 300,000/- kwa mchezaji bora wa mwezi kutoka katika kikosi cha Biashara United.

Tagged in:

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles