AfricaSwahili News

Ramaphosa asema atakomesha machafuko Afrika Kusini

 

Rais Cyril Ramaphosa amesema leo kuwa hatoruhusu machafuko na ghasia kutawala nchini Afrika Kusini na kudokeza kuwa wimbi la vurugu ambazo ziliharibu mamia ya maduka na kuwauwa zaidi ya watu 100 lilichochewa makusudi. 

Akizungumza katika Manispaa ya Ethekwini, ambayo inajumuisha mji wa bandari wa Durban, na ambao ulikuwa mojawapo ya maeneo yaliyoathirika pakubwa, Ramaphosa amesema uporaji huo na uchomaji moto vimeathiri pakubwa imani ya wawekezaji na kuathiri ukuaji uchumi wa Afrika Kusini. 

Amesema serikali yake inafanya kila liwezekanalo kutuliza hali hiyo. 

Katika taarifa yao kwa kamati ya bunge, polisi imesema uporaji bado unaendelea na maduka yanayomilikiwa na wageni yanavamiwa. 

Mikoa ya Gauteng na KwaZulu-Natal bado ni tete na watu wamekusanyika katika mikoa ya Cape Mashariki, Cape Kaskazini na Cape Magharibi.

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.