AfricaSwahili News

RC Nyerere apiga marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima Manyara

Na John Walter-Manyara.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere amepiga marufuku mikusanyiko yote isiyo ya lazima kama njia ya kukabiliana na maambukizi ya wimbi la tatu ya virusi vya corona.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 22,2021 ofisini kwake, mkuu huyo wa mkoa amesema uamuzi huo unatokana na ukweli kwamba ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya corona upo na unaua japo katika mkoa wa Manyara hakuna kisa kilichoripotiwa.

Aidha ameviomba vyombo vya habari kusaidia kutoa elimu kwa umma kuhusu kanuni za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona kunusuru maisha ya watu na kueleza kuwa wataalamu wa afya watazidi kutoa elimu maeneo yote ya mkoa huo.

Amesema iwapo kuna watu wana harusi au sherehe nyingine ambayo lazima lihusishe mikusanyiko, wahakikishe wanapata vibali kutoka ofisi za wakuu wa wilaya ambao ndio wenye mamlaka hiyo ambapo watapewa utaratibu ambao utazingatia kanuni za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona kwa mujibu wa maelekezo ya wataalam wa afya.

Nyerere amekumbusha wananchi kutii kanuni za afya zinazosisitizwa na wataalamu wa afya kwa kuwa ni muhimu kujikinga na kuwalinda wengine pia. 

Amesema Ugonjwa wa COVID-19 huenezwa  kwa matone,  Virusi huingia mwilini kupitia mdomo au pua  aidha kwa kupumua matone yaliyo ambukizwa na corona au kwa kugusa sehemu au vifaa vilivyo na virusi vya Corona.  

Hatua kama  kunawa mikono mara kwa mara, na kufunika mdomo na pua unapopiga chafya na kukohoa zinaweza kusaidia kujikinga na maradhi haya.  

 

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.