Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

RC Tabora awataka wahitimu wa JKT operesheni Samia Suluhu kuendeleza uzalendo watakapokua vyuo

Advertisement Scroll To Keep Reading

WAHITIMU  wa Mafunzo ya Awali ya Kijeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria chini ya operesheni Samia Suluhu wametakiwa kuwa mfano wa uzalendo na kuigwa watakapojiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati akifunga mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria chini ya operesheni Samia Suluhu.

Alisema wawapo Vyuoni wanatakiwa kuwa mabalozi kwa kuonyesha na kuendeleza uzalendo waliofundishwa Msange JKT ili wawe tofauti na Vijana ambao hawakubahatika kupata mafunzo.

Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Operesheni kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Aisha Matanza alisema wahitimu hao wanatakiwa kuwa macho na masikio ya Watanzania dhidi ya maadui wa ndani na nje wa Tanzania.

Alisema wantakiwa kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya maslahi ya Nchi na Watanzania na kuwa tayari kuitumikia nchi katika maeneo mbalimbali kwa uzalendo.

Kamanda wa Kikosi cha Msange JKT Kanali Sadick Mihayo alisema wahitimu hao walianza mafunzo Mwezi Juni mwaka huu wakiwa 1,533 lakini walifanikiwa kuhitimu ni 1,503.

Alisema katika cha mafunzo wahitimu hao wamefundishwa kozi za awali za kijeshi, shughuli za ujenzi , ujasiriamali kama vile utengezaji wa sabuni , ufugaji wa nyuki , michezo , maandalizi ya mashamba na shughuli za utamaduni.

Kanali Mihayo alisema mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali za kujitegemea.

Akisoma risala kwa niaba ya wenzake Caroline Tibamanya aliiomba Serikali kuongeza muda wa mafunzo kwa Mujibu wa Sheria ili wahitimu wengi waweze kunufaika na elimu inayotolewa na JKT.

 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.