Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Rouhani afichua ukweli kuhusu utawala wake

Advertisement Scroll To Keep Reading

 

Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema hakufichua “ukweli” kwa umma kwa madai kwamba utadhuru umoja wa kitaifa.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Kulingana na televisheni ya serikali ya Iran, Rouhani alitathmini urais wa miaka 8 katika hotuba yake baada ya mkutano wa baraza la mawaziri la serikali ya 12.

Rouhani alisema katika hotuba hiyo,

“Mkutano wa leo ulikuwa mkutano wa baraza la mawaziri la mwisho la serikali ya awamu ya 12. Katika muktadha huu, ni hotuba ya mwisho niliyotoa. Maneno tuliyoyatoa kwa umma katika miaka iliyopita hayakuwa ya ukweli. Sikuelezea kwa kina. ”

Akibainisha kuwa hali ya uchumi ilikuwa nzuri kutokana na ushirikiano wao na ulimwengu wakati wa kipindi cha kwanza cha urais wake (2013-2017), Rouhani alisema kuwa hali hii ilibadilika baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia mnamo 2018 na kwamba wao walijikuta katika vita vya kiuchumi na kuwekewa tena vikwazo.

Akisisitiza kwamba licha ya juhudi za serikali anayoongoza, baadhi ya mambo nchini yanazuia kuondolewa kwa vikwazo Rouhani aliendelea kwa kusema,

“Ikiwa kungekuwa na mshikamano zaidi wa kitaifa ,  mashirika mengine ya serikali yangeunga mkono serikali kwa ushirikiano, hali nchini ingekuwa nzuri.”

Rais Rouhani aliomba msamaha kwa umma kwa makosa yake na akawashukuru wajumbe wa baraza la mawaziri.

Mwanasiasa İbrahim Reisi, ambaye alishinda uchaguzi wa urais uliofanyika Juni, anatarajiwa kuchukua wadhifa kutoka Rouhani na sherehe itakayofanyika tarehe 3 Agosti.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.