Rwanda imeanza zoezi la kutoa chanjo ya pili aina ya AstraZeneca kwa wananchi wa nchi hiyo ambao awali walikuwa wamepewa dozi ya kwanza ya chanjo hiyo dhidi ya virusi vya Corona. Serikali ya Rwanda ipo mstari wa mbele katika nchi za kiafrika ambazo zinaendelea kuongoza katika kuwapatia chanjo kwa idadi kubwa ya wananchi wake.

Watu wanaopewa chanjo hii ya AstraZeneca katika zoezi lililoanza mwishoni mwa wiki ni wale ambao walichomwa dozi ya kwanza mwezi Machi mwaka huu. Awali wananchi hawa walitakuwa kuchomwa dozi ya pili ya AstraZeneca wiki nne baada ya chanjo ya kwanza kukamilika lakini haikuwezekana kutokana na sababu zisizozuilika, wizara ya afya nchini Rwanda ilisema.

Tagged in: