By Ramadhan Elias

MASHABIKI wa Simba wameshtushwa na chama lao kuanza Ligi Kuu Bara kwa suluhu dhidi ya Biashara United katika pambano lililopigwa juzi Uwanja wa Karume mjini Musoma, lakini fasta wadau wa wakawavisha mabomu nyota wapya kwa ajili ya mechi ya pili ya ugenini kesho Ijumaa dhidi ya Dodoma Jiji, sambamba na nyingine za msimu huu.

Wadau wa Simba waliozungumza baada ya mchezo huo uliokuwa wa kwanza kwa Biashara kuvuna pointi kwa Mnyama tangu walipopanda daraja msimu wa 2018-2019, walisema wachezaji wapya akiwamo Pape Sakho, Peter Banda, Henock Inonga, Sadio Kanoute na Duncan Nyoni ambao ni wa kigeni na wazawa kama Yusuph Mhilu, Israel Mwenda, AbdulSamad Kassim, Kibu Denis, Jeremia Kisubi na Jimmyson Mwanuke wakaze buti ili kuhakikisha Simba inatetea ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

Inonga, Sakho, Banda, Duncan Mhilu na Mwenda walicheza dhidi ya Biashara United na wadau kuona viwango vyao huku Kanoute, Kibu walicheza Simba Day dhidi ya TP Mazembe na baadaye Kanoute akacheza tena Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga kabla ya kuumia na kutolewa uwanjani. Mwanuke, Kisubi na Samad bado hawajacheza, lakini wadau akiwamo nyota na kocha wa zamani wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni walisema wageni ni lazima wapambane kuibeba timu.

“Sio wabaya, kila mmoja kwa niliowaona ana hadhi na uwezo wa kucheza Simba, ila wanatakiwa kujitoa zaidi. Lazima watambue Simba ni timu kubwa na mashabiki wake muda wote wanahitaji ushindi tu,” alisema Kibadeni.

Kocha msaidizi wa Simba Queens, Matty Mseti alisema wachezaji wa Simba ni bora zaidi, hivyo hana shaka juu ya kuisaidia timu hiyo kutetea ubingwa, licha ya kuanza msimu kwa suluhu dhidi ya Biashara.

Naye kocha wa Biashara United Patrick Odhiambo alisema kama wachezaji wa Simba waliojiunga watazoeana na wale waliowakuta itakuwa moto kuliko msimu uliopita.

Advertisement

News Source link

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles