By Robert Kakwesi

Tabora.  Seminari ya Itaga, imewaomba waliosoma katika shule hiyo kusaidia ukarabati wa majengo yake ambayo hivi sasa yamechakaa.

Wito huo umetolewa leo, Jumapili Oktoba 11, 2021 na Padri Joseph Buhili, amesema litakuwa jambo jema kwa wale waliosoma katika shule hiyo na wengine wenye mapenzi mema kusaidia ukarabati kwakuwa majengo hayo yaliyojengwa mwaka 1948 yanahitaji kukarabatiwa.

Amesema ukarabati huo unapaswa kufanyika hivi sasa wakati wakielekea kutimiza miaka 100 tangu shule hiyo ianzishwe

“Kuna uchakavu wa sakafu,nyaya na dali zinazoanguka na hii ni kutokana na majengo kuwa ya muda mrefu”Amesema

Ameongeza kuwa seminari ya Itaga haitoi tu mapadri Bali hata viongozi wanaokwenda kutoa mchango wao kwa jamii.

Katika kuonyesha kuguswa na ukarabati huo, Tanzania Commercial Bank imetoa msaada wa mifuko 50 ya saruji huku Meneja wa benki hiyo tawi la Tabora,Timony Joseph,amesema kilichowasukuma kutoa msaada huo ni kutambua mchango wa seminari hiyo kwa Taifa.

Advertisement

Benki hiyo pia imetoa saruji mifuko 50 kwa Kanisa Katoliki parokia ya Ipuli kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kanisa kubwa litakaloinguza waumini elfu nne kwa wakati mmoja.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles