Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Serikali Kuja Na Wiki Ya Uchanjaji

Advertisement Scroll To Keep Reading

 

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali inaandaa kampeni ya wa ‘wiki ya uchanjaji’ ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzoni mwa mwezi Oktoba kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuhusu chanjo.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Msigwa emeeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma na kusema kuwa lengo Kampeni hiyo ni kupeleka chanjo vijijini ili Watanzania wengi waweze kuipata.

“Tutakuwa na wiki ya uchanjaji, ambapo viongozi wa nchi nzima watashiriki kwenye wiki hivyo kuhakikisha watanzania wengi wanapata chanjo” amesema Msigwa,

Ameeleza kuwa wataalamu wa afya wamesema watu ambao hawajachanjwa, wakiugua Uviko-19 wanapata madhara makubwa na wengine wanapoteza maisha lakini waliochanjwa wanatibiwa na wanarudi na kurudi katika hali ya kawaida.

Kuhusu mwenendo wa chanjo, Msigwa amesema, “tumefika asilimia kama 34 ya zile chanjo milioni 1,054,400 zilizoletwa. Watanzania takribani laki 345,000 wameshapata chango hiyo, lakini pia Serikali inaendelea kuangali namna ya kuleta chanjo zingine ili watanzania waweze kupata chanjo”alisema Msigwa.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.