More
  - Advertisement -

  Serikali kupiga tafu Taifa Stars

  -

  - Ad Keep reading below -

   KATIBU Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali imejipanga kuisaidia timu ya taifa ya Tazania, Taifa Stars kwa kuipatia fedha ili kuongeza ufanisi wa timu hiyo ndani na nje ya nchi.

  Abbasi amesema hayo Mei 3, 2021 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Alfred Kidao.

  - Ad Keep reading below -

  Viongozi hao wamezungumzia namna ya kuiwezesha Stars kwenye maandalizi ya michuano ya awali ya kufunzu Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni hadi Agosti 2021.

  “Ili kupata matokeo mazuri wachezaji wetu lazima wawe vizuri kifedha hii itawasaidia kisaikolojia kuweza kupata matokeo mazuri.” Amesema Abbasi.

  - Ad Keep reading below -

  Ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuanzisha vyanzo mbalimbali vya mapato kwa ajili ya michezo ikiwemo kurudisha mchezo wa Bahati Nasibu (Sport Betting Nationary Lottary).

  ALSO READ  VIDEO: Rais Magufuli amteua Mwigulu Nchemba

  Kwa upande wake Kidao amesema maandalizi yote yamekamilika huku akieleza kuwa changamoto iliyobaki ni ukosefu wa rasilimali fedha ambapo ameshukuru namna Serikali inavyojipanga kukabili changamoto hiyo ikiwemo kusaidia posho za wanamichezo kutolewa mapema.

  ALSO READ  Sababu ya Mbowe kuitwa Polisi yatajwa

  Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania Yusuph Singo.

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Jumuiya ya kimataifa yaelezea wasiwasi juu ya ghasia za Jerusalem

   Jumuiya ya kimataifa imeelezea wasiwasi mkubwa juu ya ghasia zinazoendelea mjini Jerusalem, siku moja baada ya makabiliano baina ya polisi wa Israel na Waplestina...

  Red Cross lacking partnership of Taraba Govt – Scribe

  The leadership of the Taraba State branch of the Nigeria Red Cross has lamented what it called the lukewarm attitudes of the state government...

  Filming of Disney sequel Disenchanted to begin in Irish locations on Monday

  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -
  %d bloggers like this: