Swahili News

Serikali yaongeza posho za safari hadi Sh250,000 kwa siku

posho pc data

By Anna Potinus

Dar es Salaam. Serikali imetoa kibali cha kurekebishwa kwa posho ya kujikimu safarini kutosha Sh120,000 hadi Sh250,000 kwa daraja la juu na Sh80,000 hadi Sh100,000 kwa daraja la chini.

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa Mei 27, 2022 na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishhi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro.

“Rais Samia amebadilisha pia kiwango cha malipo cha kazi maalumu kwa ngazi ya chini kutoka 15,000 hadi Sh30,000 kwa ngazi ya kazi kutoka Sh20,000 hadi Sh40,000 na ngazi ya juu kutoka Sh30,000 hadi Sh60,000”. amesema.

Dk Ndumbaro asema kuwa mabadiliko hayo yataanza rasmi Julai Mosi, 2021 na kwamba bajeti iliyopangwa ndiyo itakayotumika kutekeleza viwango hivyo.

JOIN US ON TELEGRAM

Pia ametoa wito kwa wafanyakazi wa umma kufanya kazi kwa bidi zaidi bila kusubiri kusimamiwa, kujituma, kuwa wabunifu na wenye nidhamu na maarifa.

This article Belongs to
News Source link

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button
Muhabarishaji News We would like to show you notifications for the latest news and updates.
Dismiss
Allow Notifications

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker