More
  - Advertisement -

  Serikali yawahakikishia TABOA kumaliza kero ambazo ni kikwazo kwao

  -

  - Ad Keep reading below -

  Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

  Serikali imewahakikishia chama cha wamiliki wa mabasi hapa nchini TABOA kuwa itahakikisha inatatua na kumaliza changamoto zote ambazo ni kikwazo kwa wafanyabiashara hao ikiwamo mfumo mpya wa ukatishaji tiketi mtandao.

  - Ad Keep reading below -

  Huku ikizitaka taasisi zinazosimamia usafirishaji kuhakikisha wanatatua kero na malalamiko yanayohusu wasafirishaji kwa wakati pindi zinapofika ofisini kwao.

  Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa uchukuzi Mhe. Mwita Waitara alipokutana na chama cha wamiliki wa mabasi hapa nchini TABOA kwa lengo kusikiliza kero mbalimbali zinazowakumba katika biashara zao.

  - Ad Keep reading below -

  Ambapo amesema Serikali inania nzuri ya kuhakikisha wafanyabiashara wa mabasi wanafanyakazi bila ya kuwa na vikwazo kwani wao ni moja ya sekta muhimu ya kuchocheo uchumi hapa nchini.

  “Serikali inania nzuri sana na lengo lake ni kuhakikisha ninyi mnafanyakazi kwa uhuru ndio maana leo nimekuja hapa niwasikilize nini kikwazo kwenu kwa kuwa sekta yenu ni muhimu sana kuwasafirisha wananchi ili nao walipe kodi nchi ijiendeshe” amesema Waitara.

  ALSO READ  Picha: Rais Magufuli alivyowasili Uwanja wa Nelson Mandela

  Ameongeza kuwa “Nimewasikiliza kero zenu zote niwahakikishie tu kero zenu zote zitafanyiwa kazi hata hii kelele ya muda mrefu ya tiketi mtandao tutalifanyia kazi kwa kuwa taarifa ni kwamba mfumo unafanyiwa marekebisho bado haujawa rasmi utaboreshwa” amesema.

  ALSO READ  Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 latokea Iran

  Ameitaka Mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini LATRA kuhakikisha kero, changamoto na malalamiko mbalimbali ya TABOA yanafanyiwa kazi haraka pia wajenge utaratibu wa kusikiliza kero na kuzijibu kwa wakati ili sekta ya usafirishaji iweze kukua hapa nchini.

  - Ad Keep reading below -

  “Nimepata ushahidi hapa kwa barua mbalimbali kutokujibiwa na mimi mwenyewe shahidi kuna taarifa yangu niliomba haijafanyiwa kazi pia kuna mbunge mwenzangu katuma maombi ya kubadilisha tu rout(njia) lakini mpaka leo haijajibiwa shida ni nini” amesema.

  Aidha Mhe. Waitara amesema atahakikisha anawakutanisha LATRA na TABOA ili malalamiko yao yote yaweze kujibiwa moja kwa moja ili changamoto hizo ziweze kuondoka kabisa sambamba na hilo ili LATRA waweze kuwapitisha katika mfumo huo ili TABOA waweze kuelewa namna mfumo huo unavyofanyakazi na malengo ya kuanzishwa kwake.

  ALSO READ  Uingereza yasema kutakuwa madhara iwapo Iran haitaachia meli yake

  Awali wajumbe wa TABOA wameiomba serikali kuitazama upya LATRA na muundo wake kwani kanuni zao nyingi si rafiki kwao zinaweza kupelekea kupoteza mitaji yao kwa kufilisika kutokana na makato mengi katika biashara hiyo.

  ALSO READ  Uingereza yasema kutakuwa madhara iwapo Iran haitaachia meli yake

  Pia wamesema mfumo wa tiketi mtandao wao ndio waanzilishi lakini sasa imekuwa tofauti na malengo ya kuanzishwa kwake kwa sasa imekuwa mwiba kwao hasa baada ya kutakiwa kujaza flot kabla ya kuanza kufanyakazi na kuwa na utitili wa makato tofauti na mashine nyingine za kutolea lisiti.

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Shocking Leicester display raises serious questions about ability to handle pressure

  Leicester's top-four hoodoo returned as they collapsed in the 4-2 loss to Newcastle United.

  Postpone LG election to avoid another legal gymnastics – ex-Oyo Gov, Alao-Akala tells Makinde

  A former Governor of Oyo State, Chief Christopher Adebayo Alao-Akala, has advised the incumbent Governor, Engineer Seyi Makinde, to without wasting more time, postpone...

  FBI hails EFCC for efforts on global crime war

  The Federal Bureau of Investigation (FBI) considers the Economic and Financial Crimes Commission (EFCC) a critical partner in the global fight against organized crime...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -
  %d bloggers like this: