Mwanamuziki Shakira amesema alishawahi kuvamiwa na nguruwe pori alipotembelea hifadhi ya Barcelona akiwa na mtoto wake wa miaka nane.

Mwanamuziki huyo wa Colombia amesema wanyama hao walimvamia kabla ya kumpora begi lake na kwenda nalo msituni.

Alieleza simulizi hiyo katika mfululizo wa simulizi zake kwenye ukurasa wake Instagram, siku ya Jumatano.

Akiwa ameshikilia begi lake lililoharibiwa mbele ya kamera , alisema: “Angalia jinsi nguruwe pori wawili wa porini walivyonishambulia katika hifadhi ambako niliacha begi langu.”

“Walikuwa wamelichukua begi langu na kulitelekeza porini , na simu yangu ya mkononi ilikuwa ndani ya begi hilo ,” mwanamuziki huyo aliendelea kueleza. “Wameharibu kila kitu.”

Alafu akamgeukia mtoto wake wa kiume, ambaye baba yake ni mchezaji kandanda wa Barcelona Gerard Piqué, na alisema: “Milan waambie ukweli. Sema jinsi mama yako alivyopambana na mnyama pori.”

Hata hivyo mwaka 2016, polisi wa walipokea simu 1,187 kuhusu nguruwe hao kushambulia mbwa, paka na kusababisha foleni za magari barabarani.