Mamlaka katika mji mkuu wa Sudan imepunguza idadi ya masaa ya kufanya kazi pamoja na idadi ya masomo kwa siku kutokana na upungufu wa mkate.

Mkurugenzi wa msomo ya msingi katika jimbo la Khartoum amesema kwamba upungufu huo utaendelea hadi pale hali itakapoimarika.

‘Kutokana na hali ambayo taifa inakabiliana nalo la ukosefu wa Mikate, imeamriwa kwamba kazi shuleni zitafanywa majira ya asubuhi kutoka mwendo wa saa moja na nusu hadi saa tano na nusu asubuhi, na idadi ya masomo haitakuwa zaidi ya nne kwa siku’, Hamaza Ahmed Mohammedal-fahal alisema katika barua.

Amri hiyo iliotolewa siku ya Jumatatu inaanza kufanya kazi mara moja.

BBC imebaini kwamba kampuni za kupika mikate mjini Khartoum huenda zikakabiliwa na ukosefu wa unga wa ngano katika siku saba zijazo.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles