in ,

Siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani

Leo ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, huku kaulimbiu ya mwaka huu ikisema ”Habari kwa Faida ya Umma”. 

Kaulimbiu hii inasisitiza umuhimu usiopingika wa habari iliyothibitishwa na ya kuaminika. Inatoa wito wa kuzingatia jukumu muhimu la waandishi habari kuwa huru na kufanya kazi kwa weledi katika kutoa na kusambaza habari. 

Katika kuadhimisha siku hii DW imetoa Tuzo ya Uhuru wa Kujieleza kwa mwandishi wa Nigeria, Tobore Ovuorie mwandishi wa habari za uchunguzi. Ovuorie amekuwa akipigania kupaza sauti kwa jamii ya wasiosika nchini Nigeria. 

Ujasiri wake karibu uyagharimu maisha yake kutokana na kuandika taarifa zinazohusu wahalifu wanaohusika na biashara haramu ya watu na biashara ya viungo vya binadamu.

DR YEGERA NI BINGWA NA MTAFITI WA TIBA ASILI ALIYEJALIWA KUWA NA HOFU YA MUNGU

Coastal wakanusha, kumfuta kazi kocha Mgunda