Advertisement Scroll To Keep Reading
Michezo (Swahili)Swahili News

Simba yamwaga mamilioni Mwananyamala – Mwanaspoti

Advertisement Scroll To Keep Reading

By Clezencia Tryphone

Advertisement Scroll To Keep Reading

UONGOZI wa klabu ya Simba umetoa Sh10 milioni kwenye Hospitali ya Rufaa Mwananyamala wodi ya mama na mtoto kwaajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto.
Simba imetoa kiasi hicho cha fedha ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Simba Day, Septemba 19 kama ambavyo ufanya kila mwaka hutoa kwa jamii yenye uhitaji.
Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema mwaka huu wameamua kutoa fedha badala ya vitu ili kutoa wigo kwa uongozi wa Hospitali kununua vitu ambavyo vinahitajika kwa haraka.
 “Uongozi ndiyo unajua kitu gani kinahitajika kwa haraka na kiasi cha fedha tulichotoa kitasaidia sehemu fulani ingawa tunajua hakitaweza kumaliza kabisa tatizo,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Katibu wa Hospitali, Lilian Mwanga ameupongeza uongozi wa klabu kwa msaada huku akiutaka uhusiano huo kuendelea na usiishie leo na kwamba fedha hizo zotatumika kama ilivyokusudiwa.

“Kwa niaba ya Uongozi wa Hospitali naipongeza Simba kwa msaada huu, mnaweza kuuona kama ni mdogo lakini kwetu ni mkubwa na tutaenda kuutumia kama ilivyokusudiwa na tunawakaribisha wakati mwingine,” amesema Lilian.News Source link

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.