AfricaSwahili News

Simbachawene amtaka bosi wa NIDA ajitathimini

Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, amesema tangu ameanza kupiga kelele kuhusu vitambulisho vya NIDA hadi sasa vilivyozalishwa ni milioni 2 tu na kusema hali hiyo hawezi kuivumilia, na kumuambia Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Anold Kihaule, kama kazi imemshinda aseme.

Kauli hiyo ameitoa akiwa mkoani Iringa, na kumtaka Mkurugenzi huyo ajitathimini kuhusu suala la vitambulisho na kwamba kama anaona hawezi basi amwambie Rais Samia Suluhu Hassan, kama ameshindwa kazi hiyo ili nafasi hiyo ichukuliwe na mtu mwingine.

“Kwahiyo tangu nimeingia kwenye uwaziri kelele zote nilizopiga kwenye vitambulisho zimezalisha vitambulisho milioni 2 tu, na mimi siwezi kukubali ninachomwambia huyo Mkurugenzi Mkuu kama hii kazi imemshinda apewe kazi nyingine na hii aachie watu wengine, sawa ni mteule wa Rais, kama imemshinda amwambie,” amesema Waziri Simbachawene.

 

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.