Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Wachimbaji wadogo wadogo Mkoani Mwanza wamemuomba Waziri wa madini leo hii alipokuwa akisikiliza kero zao Mkoani Mwanza katika ukumbi wa mkuu wa mkoa .

 Sabana Salinja ambae ni katibu wa wachimbaji wa wadogo wadogo anaetokea Mhalo mining group amesema kuwa ,Serikali ijitahidi kuwatengenezea barabara na kuwapatia umeme ili kuweka miundombinu mizuri kwa wachimbaji kwani sekta ya madini ni chanzo moja wapo cha kukuza uchumi wa Nchi.

“Waziri sisi tunaomba mtupatie mtaji tuu na mtaji wenyewe ni kutengenezea barabara na kutupatia umeme mtakuwa mmemaliza maana tunatumia majeneleta ni gharama kubwa mno kwetu hata kama ni utafutaji lazima tuangalie faida na hasara kwahiyo mkitupatia hivyo vitu mtakuwa mmetusaidia mno ili na sisi tufanye kazi katika mazingira rafiki amesema Salinja.

Mwenyekiti wa Mwanza region miners association(Mwarema) Richard Seni alipokuwa akisoma risala mbele ya Waziri wa madini Dkt.Doto Biteko amebainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni baadhi ya mabenki kutowapa mikopo kutokana na  kutokuwa na  kumbukumbu ya biashara na  kutokuwa na kinga juu ya mikopo,ushirikishwaji mdogo wa Chama hicho, tozo za Halmashauri zinazidi kuwa kubwa na uchimbaji holela.

Naye Waziri wa madini Dkt.Doto Biteko alipokuwa akijibu baadhi ya hoja ya wachimbaji amesema wachimbaji wataendelea kupunguzwa kutokana na ukosefu wa uaminifu katika biashara hiyo ili waweze kubaki na wenye Nia njema na Serikali.

“Tunataka tukaguane katika kurenyuu leseni ili tubaki wachache wale waaminifu na mkubali kuwa siyo lazima wote tupate leseni unakuta mtu anakwambia Waziri mnyime huyo utupe sisi hapana wote tunahaki ya kufanya kazi ila tatizo sisi siyo waaminifu  kuna mtu kuiva anaona raha hiyo ni roho ya wizi tutaenda tunachuujana polepole mpaka tutaisha tunataka watu waaminifu tufanye nao biashara amesema Dkt.Biteko.

Waziri Biteko amesema, Mimi naona fahari mno ninapoona msukuma,muha ameenda Nchi fulani anapata mwenyeji anamuuzia mzigo na anampatia fedha zake najisikia furaha sana sasa tuache kuwaliza wageni siyo kwamba tunawachafua wao bali tunajichafua wenyewe tutende haki tuache ujanja ujanja kutokana na hali hiyo Serikali tunakamilisha usajili wake na ikikamilika hiyo Serikali itasafirisha dhabahu iliyosafishwa tuu sijasema lini ila huko tunapokwenda.

Amesema changamoto zote amezipokea na watazifanyia kazi ili kuwarahisishia wachimbaji hao kufanya kazii kwa urahisi kwani Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu anaetamani kuona wachimbaji wakinufaika zaidi kupitia sekta hiyo na kutonyanyaswa na mtu yeyote.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles