More
  - Advertisement -

  Spika aidhinisha Machi 8 kwa kura ya kutokuwa na imani na serikali

  -

  - Ad Keep reading below -

  Spika wa bunge nchini Libya Aguila Saleh amesema kuwa bunge litazungumzia kuandaliwa kwa kura ya kutokuwa na imani na serikali mpya ya umoja wa taifa mnamo Machi 8.

  - Ad Keep reading below -

  Kupitia taarifa hapo jana jioni, Saleh amesema kuwa kikao cha bunge kitaandaliwa kuzungumzia kura hiyo mjini Sirte iwapo tume ya pamoja ya kijeshi itahakikisha usalama wa mkutano huo. 

  - Ad Keep reading below -

  Tume hiyo ya kijeshi inawaleta pamoja waakilishi watano kutoka kila upande. Saleh ameongeza kuwa iwapo hatua hiyo haitawezekana, kikao hicho kitaandaliwa katika makao ya bunge ya muda mjini Tobruk siku na wakati huo huo na kuongeza kuwa tume hiyo ya kijeshi itapaswa kuliarifu bunge mapema.

  Waziri mkuu wa muda Abdul Hamid Dbeibah, siku ya Alhamisi alisema kuwa anakabiliwa na tarehe ya mwisho ya Ijumaa kuunda serikali yake kulingana na mpangilio wa Umoja wa Mataifa. 

  - Ad Keep reading below -

  Dbeibah amesema kuwa amewasilisha kwa Saleh “maono” ya mpangilio wa baraza la mawaziri ambalo litasaidia kuiongoza Libya kwenye uchaguzi wa Desemba na kwamba majina ya mawaziri waliopendekezwa yatafichuliwa bungeni wakati wa kura ya imani.

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Niger Youths lambast Jerry Gana over comment on Governor Bello’s administration

  Niger State Youths, under the auspices of Amalgamated Youth Societies (AYS) have lambasted former Information Minister, Professor Jerry Gana for being part of the...

  Job Opportunity at TANROADS, Shift in Charge

   Shift in Charge TANZANIA NATIONAL ROADS AGENCY (TANROADS) is a Semi-Autonomous Agency under the Ministry of Works and Transport established on July 1, 2000 and...

  Miaka 4 gerezani kwa mtuhumiwa aliyewapa watu sumu

   Mtuhumiwa mmoja aliyewatilia sumu watu 8 wasio na makazi na kuwarekodi video katika jimbo la California nchini Marekani (USA), amehukumiwa kifungo cha miaka 4...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -