More
  - Advertisement -

  Spika ndugai: Pasaka ya mwaka huu ilikuwa nzuri sana hasa baada ya Simba kumpiga 4-1 AS Vita

  -

  - Ad Keep reading below -

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea leo Aprili 8, 2021, likiongozwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ambaye katika kipindi cha maswali na majibu alitupa kijembe kwa mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba kuhusu ushindi wa Simba SC.

  Akimkaribisha kuuliza swali mbunge wa Kinondoni Spika Job Ndugai amesema kuwa Pasaka ya mwaka huu ilikuwa nzuri sana hasa baada ya ushindi wa Simba wa magoli 4-1 dhidi ya AS Vita kwenye uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

  - Ad Keep reading below -

  “Niwaombe radhi waheshimiwa wabunge, lakini mtakubaliana nami Pasaka ya mwaka huu ilikuwa nzuri sana hasa baada ya mtu kupigwa bao 4-1, nashindwa kujizuia kumpa nafasi mbunge wa Kinondoni (Abbas Tarimba) asiulize swali,” amesema Spika Job Ndugai.

  Aidha mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba naye akajibu kuwa amepokea kijembe hicho huku wakiwashauri Yanga SC kuitumia kama mfano ili kuendelea kuitangaza Tanzania kimataifa.

  - Ad Keep reading below -

  “Naona kijembe kimeingia sawasawa lakini na mimi ni wapongeze kwasababu Simba SC wameisaidia Tanzania kuweza kuonekana vizuri na ule utaratibu wa kuitangaza Tanzania “Visit Tanzania” kusema kweli ni jambo linalofaa kuigwa na wenzetu wa Yanga  pindi watapofanikiwa kuingia kwenye mashindano haya,” amesema Abbas Tarimba.

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  U.S. Progress on Inequality Depends on Addressing Systemic Racism, Experts Say | Best Countries

  In the spring of 2020, as the novel coronavirus pandemic swept into the United States from Europe and Asia, a disturbing pattern emerged:...

  Global Economy Set for a Post-Pandemic Boom | Best Countries

  After suffering the worst downturn since World War II, the global economy is poised for a synchronized recovery the likes of which has...

  Canada Has Work to Do to Improve Quality of Life | Best Countries

  For the sixth consecutive year, Canada has ranked first in the U.S. News & World Report's Quality of Life ranking. Topping this list...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -