Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

SUMAJKT yaingia mkataba ujenzi wa Makao Makuu ya ofisi ya mwanasheria wa Serikali

Advertisement Scroll To Keep Reading

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi amesema Ofisi yake wamelazimika kuwapa kazi ya ujenzi wa jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali Shirika la Uzalishaji Mali (SUMAJKT)  ni kutokana na nidhamu ya  kazi na uwajibikaji mzuri wa wataalam wa Shirika hillo.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Hayo ameyasema alhamisi ya tarehe 8 Septemba 21 wakati wa utiliwaji wa saini ya mkataba wa ujenzi wa Ofisi za Mwanasheria Mkuu na Uongozi wa SUMAJKT kanda ya Kati Dodoma hafla iliyofanyika kwenye moja ya ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Amesema pamoja na imani waliyonayo kwa Shirika hilo kiutendaji  pia anaamini kazi hiyo kwa wakati na ubora na weledi wa hali ya juu kulingana na Samani ya pesa na makubaliano waliyoyaingia na Shirika hilo.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani ametoa fedha hizo za Ujenzi awamu ya pili ilikuhakikisha Mji Wa serikali Mtumba unajengwa kwa wakati uliokubalika kulingana na maelekezo yake hivyo hatuna budi kulisimamia hilo ili kutimiza malengo ya nchi.” Amesema.

Awali akizungumza kabla ya Mwanasheria Mkuu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Evaristo Longopa ambaye ndiye  aliyetia saini kwaniaba ya Ofisi hiyo amesema anaiamini sana SUMAJKT na wanaamini Ujenzi huo utaanza maramoja na watakuwa bega kwa bega na SUMAJKT hilo kuhakikisha wanafanikisha na kutoa msaada na ushauri  inapohitajika.

Jengo hilo  lenye gorofa sita linategemewa kujengwa katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma na utagharimu shilingi za kitanzania Bilioni 26.8.chini ya usimazi na ushauri wa kitaalamu kutoka Wakala Wa majengo Tanzania TBA ambaye atasimama kama Mhandisi na  Mshauri Wa Ujenzi huo .

Naye Meneja Ujenzi Wa SUMAJKT Kanda ya Kati Meja Samweli Jambo alihaidi Ujenzi wajengo hilo kuisha kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika kwani SUMAJKT ni Shirika linalomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa hivyo weledi ni sehemu majukumu yao.

 Meja Jambo amesema Shirika hilo limejipambanua kwa uwajibikaji wa hali ya juu  katika kutekeleza majukumu ya Ujenzi wa majengo mbali mbali ya Serikali, na Mashirika, Majengo ya  ya watu binafsi lakini pia kuwa na wataalam wakutosha wakuweza kumaliza kazi  hata kabla ya muda unaokuwa umepangwa.

 SUMAJKT imejikita katika shughuli za ujenzi katika Kanda mbalimbali ndani ya Tanzania zikiwemo Kanda ya Ziwa,Mashariki Nyanda za juu  na Magharibi.

 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.