Taiwan imelaani kitendo cha China cha kuingiza ndege zake za kivita 38 kwenye anga yake hapo jana. Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema idadi hiyo ya ndege ni kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa, tangu ilipoanza kuchapisha ripoti ya kuingia kwa ndege kwenye anga lake katika tovuti yake rasmi Septemba 2020. 

Imesema ndege hizo za kivita ziliingia kwenye anga yake wakati China ikiadhimisha siku ya kuanzishwa kwa taifa hilo jana Ijumaa. 

Kulingana na wizara hiyo jeshi la anga la Taiwan ilitoa onyo na iliiandaa mitambo yake ya kuzuia makombora ili kufuatilia ndege hizo. Waziri Mkuu wa Taiwan Su Tseng-chang amewaambia waandishi wa habari kwamba China imekuwa ikiliimarisha jeshi lake kwa nguvu na imedhoofisha amani ya kikanda.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles