More
  - Advertisement -

  TAKUKURU Manyara yaendelea kuwabana wala rushwa na wabadhirifu wa Mali za Umma

  -

  - Ad Keep reading below -
   

  Na John Walter -Manyara. 

  - Ad Keep reading below -

  Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilaya ya Hanang mnamo April 30,2021  ilifungua kesi tatu ambapo katika hizo kesi ya uhujumu uchumi ECC. 1/2021 inamhusu Marcel Basso Siima ambaye anashtakiwa kwa makosa ya kugushi, ubadhirifu na kuisababishia hasara serikali ya shilingi Milioni kumi na sita na laki tano.

  Inadaiwa kuwa Marcel alitenda makosa hayo mwaka 2015 akiwa Mhasibu wa halmashauri ya Hanang.

  - Ad Keep reading below -

  Kesi nyingine iliyofikishwa mahakamani hapo Aprili 30,2021 ni kesi ya uhujumu uchumi namba ECC.3/2021 inayowahusu Mkojera Philemon na Rehema Kilolo ambao wanashtakiwa kwa kula njama kugushi na kuandaa nyaraka za uongo kuonesha kwamba katika kampeni ya kitaifa ya Rubella na Surua mwaka 2014 waliwalipa watu mbalimbali kwa ajili ya zoezi hilo jumla ya shilingi milioni 5,740,000/=.

  Rehema Kilolo alikana mashtaka yake na yuko nje kwa dhamana.

  Aidha Mkojera hakuwepo mahakamani hapo hivyo hakuweza kusomewa mashtaka dhidi yake na hati ya wito wa kufika mahakamani hapo imetolewa.

  ALSO READ  Dodoma: Ndege yashindwa kutua kisa hali ya hewa
  ALSO READ  "Tunamsujudia Mwenyezi Mungu Pekee" Rais wa Uturuki

  Kesi hiyo inaendeshwa na mawakii wa Takukuru Martini Makani akisaidiwa na Evaline Onditi na ipo kwa hakimu wa mahakama hiyo Mheshimiwa Aman Shao, imepangwa kutajwa Mei 28,2021.

  - Ad Keep reading below -

  Kesi nyingine iliyofunguliwa Aprili 30,2021 ni kesi ya Jinai namba CC. 66/2021 dhidi ya Elihuruma Ikula ambaye ni mtendaji wa Kijiji cha Srop wilayani hapa kwa kuomba na kupokea rushwa shilingi laki mbili na nusu.

  Alipokea fedha hizo kutoka kwa ndugu wa mtuhumiwa aliyekuwa akimshilia katika mahabusu ya kijiji kwa madai ya kuharibu mazingira.

  Mtuhumiwa alikana makosa yake na yupo nje kwa dhamana hadi Mei 28,2021 itakapokuja kwa usikilizwaji wa awali.

  Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo na Mawakili wa Takukuru Martin Makani akisaidiwa na Eveline Onditi na inasikilizwa na Hakimu wa mahakama hiyo Mheshimiwa Aman Shao.

  Mkuu wa Takukuru Holle Makungu ametoa rai kwa mamlaka za nidhamu kuendelea kuchukua hatua za kinidhamu kwa wale wote wanaofikishwa mahakamani Kama kanuni za kudumu za utumishi wa Umma (Standing orders for the public service) 2009 na kanuni za utumishi wa Umma (Public service Regulations) 2003 zinavyoelekeza.

  ALSO READ  Mahakama yatupilia mbali maombi ya aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa

  Amesema ushirikiano wa mamlaka za kinidhamu kwa wanaaofikishwa mahamani katika mapambano dhidi ya rushwa kutawafanya watumishi hao na wengine wachache wenye nia Kama hizo kujinyenyekesha kwa mola na kuacha njia zao mbaya za kukihusisha na rushwa,ubadhirifu,uhujumi wa uchumi, Wizi wa Mali za umma na kwa kuacha njia hizo mbaya,mola wetu ataendelea kuistawisha nchi yetu.(Biblia,2Mambo ya nyakati 7:14).

  ALSO READ  Djokovic aweka rekodi michuano ya wazi Ufaransa

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Shocking Leicester display raises serious questions about ability to handle pressure

  Leicester's top-four hoodoo returned as they collapsed in the 4-2 loss to Newcastle United.

  Postpone LG election to avoid another legal gymnastics – ex-Oyo Gov, Alao-Akala tells Makinde

  A former Governor of Oyo State, Chief Christopher Adebayo Alao-Akala, has advised the incumbent Governor, Engineer Seyi Makinde, to without wasting more time, postpone...

  FBI hails EFCC for efforts on global crime war

  The Federal Bureau of Investigation (FBI) considers the Economic and Financial Crimes Commission (EFCC) a critical partner in the global fight against organized crime...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -
  %d bloggers like this: