Serikali mpya ya Afghanistan, inayoongozwa na kundi la Taliban, imewaonya wajumbe wa Marekani na Umoja wa Ulaya, kuwa muendelezo wa majaribio ya kuwawekea shinikizo kupitia vikwazo yatadhoofisha usalama na huenda hali hiyo ikasababisha wimbo wa wakimbizi wa kiuchumi.

 
 Kaimu waziri wa mambo ya kigeni Amir Khan Muttaqi, aliwaambia wanadiplomasia katika mazungumzo mjini Doha kwamba kudhoofishwa kwa serikali ya Afghanistan hakumnufaishi yeyote, kwasababu athari zake hasi zitauathiri moja kwa moja ulimwengu katika sekta ya usalama na uhamiaji wa kiuchumi kutokea nchini humo. 
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wake, Muttaqi aliuhimiza ulimwengu kupitia mkutano huo wa Doha, kuondoa vikwazo na kuziacha benki zifanye kazi yake kama kawaida ili makundi ya hisani, mashirika na serikali yaweze kulipa mishahara kwa wafanyakazi wao. 
 
Washington na Umoja wa Ulaya wamesema wako tayari kusaidia mikakati ya kiutu nchini Afghanistan, lakini wana wasiwasi juu ya kutoa msaada huo moja kwa moja kwa Taliban bila uhakikisho kwamba watawala hao wapya wataheshimu haki za binadamu, na hasa haki za wanawake.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles