AfricaSwahili News

TAMISEMI QUEENS yaichapa IHUMWA DREAM TEAM magoli 74-23

Na Mathew Kwembe, Arusha.

Ndoto za timu ya netiboli ya Ihumwa Dream kutoka Dodoma ya kufanya vizuri katika michuano ya netiboli ligi daraja la kwanza inayoendelea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ilififia leo asubuhi baada ya timu hiyo kuchapwa na timu ya TAMISEMI QUEENS   kwa magoli 74-23.

TAMISEMI QUEENS ambayo inamilikiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI pia ya Dodoma iliyapata magoli yake kupitia kwa wachezaji Lilian Jovin, na Dorice Antony wakati kwa upande wa Ihumwa yalifungwa na Dalia Rashid na Asha Khalfan.

Lilian ambaye ni mfungaji hodari wa TAMISEMI QUEENS kutokana na umahiri mkubwa wa kufunga magoli aliounyesha katika mechi tatu ambazo timu yake imecheza anatarajiwa kupigania tuzo ya ufungaji bora katika ligi hiyo.

Mchezaji aliyetia fora katika mechi ya leo ni ‘senta’ wa TAMISEMI QUEENS Semeni Abeid ambaye alikuwa akihaha uwanja mzima kuhakikisha timu yake inapata ushindi mkubwa.

Kwa matokeo hayo, timu ya TAMISEMI QUEENS imefanikiwa kujikusanyia jumla ya pointi 6 katika michezo 3 iliyocheza ambapo timu hiyo ilifanikiwa kushinda mechi zote 3.

Katika mchezo wa leo TAMISEMI QUEENS iliwapumzisha baadhi ya mastaa wake kama vile golikipa Chuki Kikalao, Sophia Komba, Flora Odilo na Aziza Itonye na kuwachezesha golikipa Rehema Juma, Mersiana Kizenga, Upendo Adrian, na Asha Rashid

Akizungumzia michuano hiyo Katibu wa TAMISEMI QUEENS Alex Ntenga amesema kuwa timu yake imejiweka katika nafasi nzuri kufuatia ushindi ilioupata mfululizo, na kwamba anaamini timu yake ina uwezo wa kuendelea kushinda kila mchezo unaokuja.

Katika mchezo mwingine uliochezwa asubuhi Maafande wa Polisi kutoka hapa Arusha walifanikiwa kuwalaza Eagles ya Dar es salaam magoli 56-22

Michuano hiyo itaendelea tena jioni kwa mchezo mkali na wa kusisimua kati ya timu za Magereza Morogoro kuchuana na Mbweni JKT.

 

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.