AfricaSwahili News

‘Tanzania hatuna wakimbizi kutoka Msumbiji’

 

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, bwana George Simbachawene amekanusha uwepo wa wakimbizi kusini mwa Tanzania .

Waziri Simbachawane amesema Tanzania kazi yake kama nchi ni kulinda mipaka yake na kulinda watu wake.

Vilevile ifahamike kuwa katika jumuiya ya kimataifa Tanzania inawahifadhi wakimbizi na waomba hifadhi zaidi ya laki mbili sabini na tano elfu kutoka nchi mbalimbali zilizopata machafuko ya kisiasa au mapigano ya wenyewe kwa wenyewe au sababu nyingine mbalimbali.

“Kazi ya taifa letu katika kulinda mipaka na nchi yake, mpaka wa kusini ambao tuapakana na Msumbiji kuna mikoa mitatu Lindi, Mtwara na Ruvuma, katika mikoa hiyo sisi hatuna wakimbizi kutoka nchi yeyote ila tunafahamu kuwa katika nchi ya Msumbiji jimbo la Cabo Delgado kuna machafuko ambayo yalifanywa na magaidi.

Magaidi wanafanya ghasia katika eneo hilo na hivyo watu wanakimbia katika maeneo mbalimbali, na katika upande wetu sisi si rahisi kuweza kuwachuja kujua huyu mkimbizi au gaidi, maana kwa macho hatuwezi kupima au kuona tofauti yao,” Simbachawene amesema.

Aidha aliogeza kusema kuwa Tanzania haijaresha wakimbizi kwa sababu haina wakimbizi kusini mwa nchi yake.

Amesema katika ukanda wa Afrika Mashariki na ukanda wa maziwa makuu, Tanzania inaongoza kwa kuhifadhi wakimbizi na wana uzoefu huo na vilevile wana heshimu sana sheria za kimataifa kwa wakimbizi lakini mpaka sasa hawana wakimbizi wa Msumbiji alisisitiza kwa kusema … “Hatuna wakimbizi kusini mwa Tanzania sasa tunawafukuza vipi!”.

Awali, Mamlaka nchini Msumbiji zimesema kuwa zaidi ya raia 9,600 wa Msumbiji wanaokimbia vurugu kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado “wamerudishwa kwa nguvu” kutoka Tanzania tangu Januari 2021, Diario de Noticias gazeti binafsi nchini humo limeripoti.

Kulingana na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa karibu watu 900 “walisukumwa kwa lazima” kuvuka mpaka kati ya tarehe 7 na 9 Juni.

Ripoti hiyo inakuja saa chache baada ya manusura walionukuliwa na tovuti inayomilikiwa na watu binafsi O Pais, kufichua kwamba mji wa Palma kaskazini mwa Msumbiji, ulibaki ukikaliwa na wanamgambo, ambao wanachama wao wanaendelea “kuchoma nyumba, kuua na kuteka nyara watu”.

Mashambulio makubwa ya hivi karibuni ya kundi hilo dhidi ya mji wa Palma mnamo 24 Machi, yaliwahamisha zaidi ya watu 70,000, na kuongeza idadi ya watu waliohamishwa kutokana na ghasia kaskazini mwa Msumbiji hadi karibu 800,000.

Mnamo mwezi Aprili Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania George Simbachewene alisema kuwa Ripoti ya Umoja wa mataifa juu ya Tanzania kurudisha wakimbizi wa Msumbuji haina uhalisia wowote.

Katika mahojiano na BBC Simbachawene alisisitiza kuwa Tanzania inalinda mipaka yake na kujilinda dhidi ya magaidi ambao wakati mwingine wanaweza kujichanganya na wakimbizi na kisha kuingia nchini.

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.