Swahili News

Tanzania na Botswana kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na mapambano dhidi ya Covid 19

Rais Mokgweetsi Masisi amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika ikulu ya Dar-es-salaam mara baada ya kuwasili Alhamisi asubuhi nchini humo na kupokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.

Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo yao ya faragha Ikulu jijini Dar-es-salaam rais Samia na Masisi wameelezea nia ya kuendeleza mahusiano zaidi ya kiuchumi na hata pia masuala ya ulinzi na usalama na mapambano ya ugonjwa wa COVID 19.Rais MASISI ni mwenyekiti wa asasi ya kisiasa ya SADC -Troika.

Rais Samia Suluhu kwa upande wake ameahidi kutumia uzoefu wa maendeleo ya kiuchumi ya nchi ya Bostwana kufanya mageuzi ya kiuchumi nchini Tanzania husasan katika sekta ya madini.

Ziara hii ya siku mbili ya rais wa Botswana imefanyika wakati urari wa kibishara kati ya Tanzania na Botswana katika kipindi cha mwaka 2020 ulifikia Shilingi bilioni 3 baada ya kupanda kutoka Bilioni 1.8 mwaka 2019 na shilingi milioni 731 kwa kipindi cha mwaka 2016.

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.