By Elizabeth Edward

Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imelazimika kuongeza muda wa udahili kwa siku tano, baada ya kukamilika kwa ratiba ya udahili ya mwaka wa masomo 2021/22, ili kutoa fursa kwa waombaji waliokosa nafasi hizo.

Kulingana na TCU, baada ya kukamilika kwa awamu zote tatu za udahili, kumekuwa na maombi ya kuongeza muda kutoka kwa waombaji wengine ambao walikosa fursa hiyo.
 
Sanjari na maombi ya waombaji taasisi za elimu ya juu nazo zimeomba kufunguliwa kwa awamu nyingine ya udahili kutokana na kuwepo kwa programu ambazo bado zina nafasi ya kupokea wanafunzi.

Akizungumza leo Oktoba 21 jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Profesa Charles Kihampa amesema wamepata maombi ya taasisi za elimu ya juu zikihitaji wanafunzi kwa ajili ya kujaza nafasi kwenye programu ambazo bado zinazohitaji wanafunzi.
 
“Tumepata maombi kutoka kwenye vyuo na tukaona tutoe hiyo grace period (kipindi msamaha) ya siku tano watu watume maombi kisha taratibu zingine za vyuo kwenye udahili ziendelee na watatoa orodha ya majina waliodahiliwa kwenye awamu huu ya nne.
 
“Kuhusu programu vyuo ndio vinafahamu ila kwa kuwa kuna orodha ya programu na idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kudahiliwa kwa mwaka huu, ni lazima idadi hiyo ifikiwe,” amesema Profesa Kihampa Kihampa.
 
 
Kwa mujibu wa Profesa Kihampa kwa mwaka huu wa masomo kumekuwa na ongezeko la nafasi  kufikia 164,901 za ikilinganishwa na 157,770 katika mwaka wa masomo 2020/21 ambayo ni ongezeko la nafasi 7,131 (asilimia 4.5) huku programu 724 zikitarajiwa kutolewa mwaka huu.
 
 
“Ili kutoa fursa kwa waombaji ambao hawajakubaliwa au hawajaweza kuomba udahili katika awamu tatu zilizopita, tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua dirisha la nne na la mwisho la udahili ambalo linaanza leo (jana) Oktoba 11 hadi Oktoba 15, 2021,” amesema Profesa Kihampa.
 
Alisema waombaji wote ambao bado hawajakubaliwa kutumia vizuri fursa hiyo kupata udahili kwani hakutakuwa na nyongeza zaidi baadaye.
 
Pia, Profesa Kihampa amewahimiza wanafunzi ambao wameandikishwa katika vyuo zaidi ya moja na hawajajithibitisha katika taasisi yoyote kufanya hivyo kabla ya Oktoba 24 mwaka huu.
 
Wiki iliyopita Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako alieleza kutoridishwa kwake na idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kwenye taasisi za elimu ya juu na kuzitaka kuongeza miundombinu ili kudahili wanafunzi wengi zaidi.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles