Michezo (Swahili)

TFF yatoa tamko kuhusu mechi ya Simba na Yanga

Shirikisho ka Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na kilichotokea na kusababisha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ifanyike jana iahirishwe.

TFF inapenda kuomba radhi kwa wadau wote, waliolipa viingilio kuingia uwanjani, waliokuwa wakisubiria kuangalia kwenye televisheni, kusikiliza redioni na watoa huduma mbalimbali.

Kwa hali hiyo TFF imetoa maelekezo kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutoa taarifa kwa kina kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo, pamoja na kushughulikia hatma ya wapenzi wa mpira wa miguu waliolipa viingilio kuingia uwanjani.

Show More

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.