AfricaSwahili News

Treni yenye kasi zaidi duniani yazinduliwa China

Treni hiyo ya mfumo wa Magliev iliotengenezwa na shirika la reli nchini China inadaiwa kuwa yenye kasi zaidi duniani CRRC.

‘’Magliev ni neno kwa ufupi lenye maana ya magnetic Levitation’’.

Treni hiyo inaonekana kuolea angani kutokana na nguvu za umeme zinazoifanya kuonekana kuwa juu ya barabara ya reli.

Liang Jianying, naibu meneja na muhandisi mkuu wa shirika la CRRC Sifang , aliambia vyombo vya habari nchini humo kwamba mbali na kasi yake , treni hiyo haina kelele na inahitaji uangalizi mdogo ikilinganishwa na treni zengine zenye kasi ya juu

Mfano wa treni kama hiyo ulifichuliwa kwa vyombo vya habari mwaka 2019.

Mwaka huohuo, China ilitangaza mipango yake ya kuanzisha uchukuzi wa saa 3 katika katika miji yake mikuu.

Reli yenye kasi ya juu nchini China ni kipaumbele , ikiwa na lengo la kuunganisha miji yake mikuu kwa treni ili kupunguza muda na gharama za usafiri ndani ya taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu duniani.

Kwa sasa , wastani wa kasi ya treni nchini humo ni kilomita 350 kwa saa , huku ndege zikiendeshwa katika kasi ya kati ya kilomita 800 hadi 900 kwa saa.

Treni kama hiyo iliozinduliwa Qingdao inaweza kujaza pengo muhimu lililopo katikati.

Hatahivyo kuna kitu kimoja muhimu ambacho ni kizuizi katika ufanisi wake – ukosefu wa reli za magliev ambazo hazijakamilishwa.

Kwa sasa China ina reli moja pekee ya mfumo wa Magliev inayotumika kibiashara, na inaunganisha uwanja wa ndege wa Pudong huko Shanghai na kituo cha barabarani cha Longyang mjini humo.

Safari hiyo ya kilomita 30 huchukua takriban dakika saba na nusu huku treni hiyo ikisafiri kwa kasi ya kilomita 430 kwa saa moja.

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.