Wakati Miamba ya soka Afrika Mashariki na Kati, Mabingwa wa Nchi na wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC wakijiandaa kuikabili timu ya Jwaneng Galaxy Football Club ya Botswana tarehe 17/10/2021 pale katika Uwanja wa Galax, wadau mbalimbali wamekuwa wakiitazamia mechi hiyo kwa jicho la kipekee. Mchambuzi wa soka Abbas Pira kwa upande wake amesema kuwa Simba SC itaondoka na alama tatu pale Galax na inayo nafasi kubwa ya kuchukua point hizo kwenye mchezo wa marudiano 24/10/ 2021 hapa nyumbani kwenye uwanja wa Mkapa.

”Simba itashinda Botswana kwa sababu kocha Gomes amekutana na mechi nyingi kubwa kabla ya kukutan na Jwaneng Galaxy, lakini pia wanawachezaji wazuri hivyo watafanya vizuri huko Botswana na hata hapa Dar es Salaam.”- Abbas Pira

Tagged in:

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles