Serikali ya Ufaransa imemuita ili kumuhoji Rais wa Baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini Ufaransa, aliyesema mapadri hawatakiwi kwenda polisi baada ya kuungama kuhusu visa vya unyanyasaji wa watoto, wakati wa sakramenti ya kitubio, akisema suala la kuungama liko juu ya sheria za taifa hilo.

Askofu Eric de Moulins-Beaufort atatakiwa kufika mbele ya waziri wa mambo ya ndani Gerald Darmanin mapema wiki ijayo kutolea maelezo matamshi hayo, baada ya Rais Emmanuel Macron kumuagiza waziri huyo kufanya hivyo. 

Askofu huyo alitoa kauli hiyo baada ya uchunguzi wa serikali kufichua kiwango kikubwa cha visa vya unyanyasaji wa kingono kwa watoto katika kanisa Katoliki nchini Ufaransa.

Amesema maungamo yanapaswa kubaki kuwa siri kwa sababu yanafungua nafasi ambayo mtu anaweza kuzungumza kwa uwazi mbele ya Mungu. Takriban wahanga 216,000 walidhulumiwa kingono kwa zaidi ya miaka 70, unyanyasaji ambao haukuripotiwa.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles