Uhispania imesitisha mchakato wa kutoa chanjo ya AstraZeneca iliyoboreshwa dhidi ya corona (Covid-19) kwa watu walio na umri wa chini ya miaka 60, kutokana na madai ya utata yanayohusu athari mbaya yaliyoenea barani Ulaya.
Katika mkutano na idara za afya za tawala 17 za maeneo huru nchini Uhispania, Waziri wa Afya wa Uhispania Carolina Darias alisema kwamba walipendelea kuchukua uamuzi tofauti licha ya pendekezo la Shirika la Dawa la Ulaya (EMA) la “kuendelea kutumia AstraZeneca kwa misingi kwamba faida zake ni zaidi ya hatari zake, ingawa kuna uwezekano wa kusababisha tatizo la kuganda kwa damu.”
Wizara ilisitisha chanjo hiyo kutolewa kwa watu walio na umri wa chini ya miaka 60, bila kubainisha tarehe.
Hata hivyo, imetangazwa kuwa chanjo ya AstraZeneca inaweza kutolewa kwa hiari kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 60.
Baadhi ya nchi za Ulaya kama vile Ubelgiji na Italia, pia zilitangaza kusitisha utoaji wa chanjo hii kwa watu walio na umri wa chini ya miaka 60.