Wanasiasa nchini Ujerumani leo wataanza juhudi za kuunda serikali mpya baada chama cha siasa za wastani za mrengo wa shoto SPD kupata ushindi mwembamba katika uchaguzi uliofanyika jana ambao umeshindwa kutoa mwelekeo kamili wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya. 

 
Viongozi wa vyama vilivyopata nafasi ya kuingia Bungeni wanakutana leo kutathmini matokeo ya uchaguzi ambayo yameshuhudia muungano wa vyama vya CDU/CSU wa Kansela Angela Merkel ukipata matokeo mabaya zaidi katika historia ya uchaguzi wa shirikisho. 
 
Mgombea wa Ukansela kupitia chama cha SPD kilichojikingia asilimia 25.9 ya kura Olaf Scholz amejipigia upatu kuwa anaweza kuunda serikali inayokuja. 
 
Katika uchaguzi huo wa jana vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU/CSU vimepata asilimia 24.1 ya kura na kufuatiwa na chama cha kijani kilichopata asilimia 14.8

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles