By Fortune Francis

Dar es Salaam. Kitendo cha baadhi ya wateja kushindwa kulipa mikopo kwa wakati, kimetajwa kuwa moja ya changamoto kubwa kwa uendeshaji wa taasisi hizo za fedha nchini.
Pia, hatua hiyo imetajwa kusababisha baadhi ya taasisi hizo kupungua kwa mitaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Equity, Ester Kileo, ameeleza hayo leo Ijumaa  Oktoba, 22,2021 katika kongamano la wiki ya huduma za kifedha linaloendelea kwenye hoteli ya Serena, Dar es Salaam.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) na kushirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya fedha nchini, limedhaminiwa na benki za CRDB, NBC, NMB pamoja na Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Ester amesema kumekuwa na mikopo mikubwa ambayo kesi zake ziko mahakamani na kushauri kuwepo kwa mabadiliko kwenye mifumo ya mahakama nchini ili kuwezesha fedha hizo kurudi kwenye mabenki na kutoa fursa kwa wateja wengine kukopa na kuendeleza miradi.

Amesema zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wamejikita kwenye sekta ya kilimo na endapo watawezeshwa kwa kupata mitaji, watasaidia kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.

“Kama benki kwenye sekta ya fedha kuna haja ya kuona ni kitu gani cha kufanya ili kuendelea kuziwezesha sekta mbalimbali kuanzia ndogo hadi kubwa katika kukuza mitaji,” amesema Kileo.

Advertisement

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles