Baraza la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa limekubaliana kwa tofauti ya kura chache hii leo kuhitimisha mamlaka ya wachunguzi wake huru waliogundua kwamba pande zote kwenye mzozo nchini Yemen zilifanya vitendo vinavyoweza kutajwa kuwa vya uhalifu wa kivita. 

Kura hiyo ya wanachama 47 wa baraza hilo katika kongamano lililofanyika mjini Geneva ilihitimishwa kwa mataifa 21 kupinga azimio hilo huku 18 yakiunga mkono. 

Mataifa saba hayakupiga kura na Ukraine haikushiriki kabisa kwenye mchakato huo. Saudi Arabia ilipinga vikali azimio hilo la magharibi ambalo iwapo lingepitishwa timu hiyo ingeongezewa muda wa miaka miwili. 

Wataalamu hao walibaini uwezekano wa uhalifu wa kivita nchini Yemen ikiwa ni pamoja na uliofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Riyadh.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles